
Inasikitisha kuona gazeti kama Uwazi linachapia pale wanapotoa picha ya Randy Jackson wa American Idols kudhani kuwa ni Randy Jackson mdogo wake hayati Michael Jackson. Randy Jackson wa American Idols mara nyingi alikuwa anasema kuwa yeye ahusiani na Michael Jackson ni majina tu yamefanana, pia kiumri amemzidi Michael jackson kwa kuwa yeye kaziliwa 1956 wakati Randy Jackson mdogo wake Michael alizaliwa 1961.

Gazeti hili pia lilichapia walipotoa picha ya Randy Jackson wakisema ni Tito Jackson ambaye ni kaka ya Michael Jackson. Kwa kifupi gazeti hili haliko makini ukilisoma lazimi uthibitishe yaliomo. Labda pengine kuna mtu sasa hivi akiangalia American Idols anaweza kubisha kuwa Randy (jaji wa shindano hilo) ni mdogo wa Michael Jackson kumbe hawana undugu.
3 comments:
Aaah kaka hayo magazeti ya Shigongo we yaonage tu..! Hayana hadhi kuyaita magazeti..sababu gazeti lazima liwe na muhariri, haya magazeti ya huyu bwana mkubwa nathubutu kusema haya muhariri, huandikwa makosa ya wazi wazi, eti juzi walitwambia dola za kimarekani laki sita na hamsini nisawa na Tsh laki saba!!! Hata kama ni udaku basi uwe unaleta sense, sio kukosa umakini kiasi hata mtu unapoteza hamu ya kusoma! Mi naona Shigongo angeendelea kuandika Hadithi tu, sababu kwenye upande wa kupasha habari (za kidaku) hawezi, hana waandishi makini, wala hana wahiriri makini! Hakuna siku gazeti lake linatoka lisiwe na makosa ya kihariri au habari potofu...ni utumbo mtupu!
Kweli huyu bwana pia waandishi wake wa habari ni bomu, yani cheap labour. Ni aibu sana, anatakiwa aangalie upya safu yake ya waandishi wa habari.
Yani ni sijui nisemeje, magazeti haya yanapotosha jamii kabisa. If they cant get an obvious story right, how the hell are we going to believe the crap they have been narrating all along? Wajua Shingongo kazoea kuandia hadithi sana, sasa hata habari za maisha ya watu anataka kuzitoa kichwani.
Post a Comment