Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

March 16, 2009

UCHAFUZI WA MAZINGIRA KATIKA ENEO LA FERI

Huyu bwana sio kuwa anaosha miguu, ila ametoka kuchafua mazingira hadharani katika bahari ya hindi karibu na soko la samaki Ferry Jiji Dar es salaam.

Huyu ni mvuvi wa eneo hili la Ferry, wavuvi mara nyingi wakiona bahari hujisikia wako nyumbani, dhana hiyo "sometimes" huwapelekea kuchafua mazingira kwa kuenda haja kubwa pembezoni mwa bahari.
Huyu pia ni mvuvi mwengine ambaye anachafua mazingira, jambo hili sio zuri kabisa na inatakiwa waelimishwe na kutengewa choo ambacho kitakidhi mahitaji yao.

Wakimaliza haja yao hunawa kwa kutumia maji ya bahari kisha huendelea na kazi yao.

Mvuvi anamuekea samaki mama ambaye hufanya biashara ya kuuza samaki waliokaangwa.

Hapa ndio Mnadani katika soko la samaki.

Ukimaliza kununua samaki unawaleta hapa kwa ajili ya kupaa kisha unawaachia hela ndogo tu ni maelewano.

Ukisikia uvivu wakipika samaki unawaleta hapa hawa wamama wanakupikia ni wewetu na hela zako.

1 comment:

Anonymous said...

Jamani duh uchafu sana.