Hii ni sehemu ya ndani ambayo inawajumuisha wafanyabiashara zaidi ya 600. Soko hili lilijengwa mwaka 1974 kwa msaada wa aliyekuwa Rais wakati huwo Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Kijana Kipocho A. Kipocho akipanga bidhaa yake ya samaki aina ya Nguru na Papa.
Msukuma mkokoteni katika soko hilo akisoma kibao kilichowekwa na wafanyabishra katika soko hilo chenye ujumbe usemao kuwa hili ni eneo la wafanyabiashara sokoni Tandika eneo hilo haliuzwi na haliruhusiwi kujengwa. Polisi wamekuwa wakija hapo sokoni wakidai kuwa hawata ruhusu ujenzi uendelee pasipo kujua hatima ya wafanyabishara hao watakwenda wapi.
Moja ya notisi walizopewa na afisa mtendaji wa Kata ya Tandika ya kuwajulisha juu ya mwekezaji katika soko hilo.
.
.
Wafanyabiashara katika soko la Tandika jijini Dar es Salaam, wako katika wakati mgumu baada ya mfanyabiashara mmoja ambaye hakupatikana jina lake wala kampuni yake kulilinunua soko hilo. Barua iliyotoka Halimashauri ya manispaa ya Temeke, ofisi ya afisa Mtendaji kata ya Tandika iliyoandikwa Februari 2, 2009 yenye kumbukumbu namba TMK/TNK/127/02/09, ikiwa na kichwa cha habari Kisemacho YAH. KUMTAMBULISHAMWEKEZAJI M/S TECHNICAL DEVOLEPERS. Barua hiyo ilikuwa ikitoa maelekezokwa uiongozi wa soko kuwa tayari mtajwa hapo juu ameshinda zabuni ya kujenga maduka katika soko hilo na atajenga kwa miezi 6 na kutafuta wapangaji kwa miezi 6 hivyo kutokana na kutoa pesa zake itachukua muda wa miaka 8 kisha atalirudisha eneo hilo.
Hata hivyo soko hilo ambalo lilijengwa na Mwalimu Nyerere miaka ya 1974 aliwajengea wakazi wa eneo hilo kwa muda wote huo wananchi walikuwa wakinufaika na soko hilo, kutokana na kukodishwa kwa soko hilo jumla ya wafanyabiashara ya maduka 150 na wafanyabiashara ya meza 700 watapoteza nafasi zao kwani mkandalasi huo amepanga kujenga maduka hayo na kutafuta wapangaji wake. Hata hivyo uongozi wa wafanyabishara tayari walipeleka malalamiko yao kwa Meya wa Temeke, lakini cha kushangaza ni msimamo uliotolewa na mkuu huyo kuwa ni lazima wajenge pasipo kuwajulisha niwapi watakapokuwa wakifanyia bishara zao. Wafanyabiashara hao wameapa kuwa hawatakuwa tayari kufukuzwa katika soko hilo ambalo ni mali yao hasa wakiwa ni wazawa wa hapa nchini. Kumekuwa na vitisho kutoka kwa viongozi wa kuu hasa Mkuu wa kituo cha Polisi cha Chang'ombe kwa kuwambia kila mmoja atakamatwa na kufunguliwa shitaka lake kinyume na sheria.
No comments:
Post a Comment