
Kampuni ya bia ya Serengeti yashinda medali mbili za dhahabu katika bia za Premium Serengeti na The Kick kwa mwaka huu wa 2009. Medali hizi wamepewa na Chama cha Wakulima cha Ujerumani DLG. Deutsche Landwirtschafts Gesellschaft (DLG) iko Frankfurt na ni moja ya vyama muhimu vya kupima ubora wa vinywaji duniani. DLG ina wanachama zaidi ya elfu kumi na saba (17,000) duniani na hupima ubora wa viwango wa vinywaji zaidi ya elfu ishirini (20,000) kila mwaka.

Brew Master Ralf Schuster kushoto na Meneja Uhusiano wa kampuni ya Serengeti Breweries Teddy Mapunda kulia wakionyesha tuzo walizoshinda.

Teddy mapunda Meneja Uhusiano akionyesha medali walizoshinda.
No comments:
Post a Comment