Kijana Ibrahim Mwinyi akielekea lupango baada ya hukumu yake ya mwaka mmoja kwa kosa la kumpiga kofi Rais Mstaafu Al Haji Ali Hassan Mwinyi.
Kijana huyu alipoulizwa na waandishi wa habari kuwa amebeba nini, akajibu kuwa amebeba zawadi aliyoletewa na wa Kristo. Akaongeza kuwa siyo kweli kuwa yeye anachukiwa na wa Kristo, akasema anachukiwa na watu wa dini zote kwa kitendo chake.
Hakusema kilichokuwemo ndani ya mfuko huwo au ni zawadi ya aina gani. Hata hivyo mshitakiwa aliomba msamaha kwa serikali na Watanzania wote kwa ujumla kwa kosa alilolitenda la kumpiga kofi Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi. Hakimu aliyekuwa akiendesha kesi hiyo Neema Chusy alimsomea mshitakiwa shitaka lake na baada ya kumaliza alimpa mshtakiwa nafasi ya kujitetea. Kabla ya kujitetea alianza kuswali, hata hivyo hakimu alimkanya na kumwambia aongee kwa lugha inayoeleweka. baadaye hakimu Neema alitoa hukumu yake ya kifugo cha mwaka mmoja jela.
No comments:
Post a Comment