Chama cha wandishi wa habari za Bunge wamapata mafunzo yaliyotolewa na Ofisi ya Bunge, mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Karimjee ambapo mada mbalimbali ziliwakilishwa na wataalum toka katika ofisi za bunge. Mada ya kwanza ilitolewa na Rioba Ayubu iliyohusu Ripoti ya Maadili ya Bunge na athari ya Vyombo vya Habari katika jamii ( Ethics in Parliamentary Reporting and the Effects of the Media to the Public). Mada ya pili ilitolewa na mmoja wa maafisa wa bunge Said Yakubu, ilihusu Uandishi wa habari za Bunge Changamoto na Mapendekezo. Said aliwaambia wandishi wa habari za bunge ambao walihudhulria semina hiyo kuwa Bunge na Vyombo vya Habari vinategemeana sana kwa kuwa bila chombo cha habari kuarifu wananchi kinachotendeke Bungeni ni sawa na kusema hakuna Bunge, na pia bila Bunge ama wanasiasa kwa ujumla ni sawa na kusema chombo cha habari kutakuwa hakuna mambo mengi ya kuarifu wananchi.
.
Katika semina hiyo ambayo ni ya pili tangu kuanzishwa kwa chama cha wandishi wa habari za Bunge kilichoanzishwa mwaka jana mwezi Juni katika ukumbi wa mikutano wa St Gasper Dodoma, Said Yakubu alisema kuwa Bunge ni Mhimili wa Dola wenye kazi kuu ya kutunga sheria na kuichunguza, kuisimamia serikali na kwa upande wake wandishi wa habari ama vyombo vya habari ni mhimili wa Dola, wenye kazi kuu ya kauarifu wananchi yanayotendwa na serikali na pia kushauri njia bora ya kukabiliana na mapungufu yanayotendeke katika jamii. Hivyo aliwaomba waandishi wa habari kujenga utamaduni wa kujisomea kanuni za Bunge Hanrsard na taratibu nyingine kila wakati ili kujenga uelewa sahihi wa vitendea kazi vyao.
Mada ya Tatu iliendeshwa na Damas Ndumbaro ambayo ilihusu sheria ya Vyombo vya Habari na Bunge na Maadili na Uhuru wa Wandishi. (MEDIA AND THE PARLIAMENT LAW, ETHICS AND FREEDOM OF PRESS).

No comments:
Post a Comment