Kumetokea ujambazi maeneo ya Kariakoo sasa hivi asubuhi ambapo vijana watatu walimpora mtu aliyekuwa anaenda kupeleka hela katika duka la kubadili hela Kariakoo Bazaar Bureau De Change. Hivyo basi wizi huwo ulitokea nje ya Kariakoo Bazaar ambapo nikuribu na soko la Kariakoo. Kwa mujibu wa waliokuwa katika eneo la tukio, majambazi hao walifanya kazi yao kwa kasi kubwa na kuondoka mara moja kwa miguu na baadaye kuingia kwenye gari lililokuwa limeegeshwa eneo la Msimbazi. Majambazi hao walipigi risasi mbili hewani na kuingia kwenye gari lao ambapo kabla hawajatoweka walimgonga mtu na kutokomea kwa kupitia mtaa wa Narung'ombe. Baadhi ya watu walisikika wakisema majambazi hao walikuwa vijana wadogo sana. Polisi walifika eneo la tukio lakini majambazi walikuwa wameshatoweka kitambo.
March 17, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
















2 comments:
@DUH :-(!
tuanze kutumia credit cards
Post a Comment