Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

February 25, 2009

MTOTO ALIYETOLEWA MAHARI HUKU AKIWA AMEFAULU SHULE

Halima Likutu akiwa katika chumba cha mkutano cha benki ya posta wakati alipokuwa akiongea na wandishi wa habari.

Mama mlezi wa Halima hapa jijini Farida Dihenga akiongea jinsi matatizo yalivyomkuta mwanawe, wakati alipoongea na wandishi wa habari katika ofisi za benki ya posta ambao wameamua kumsomesha sekondari.

Head of Banking operation Posta Bank's Michael Mwakyandile akionge jambo wakati walipotoa msaada wa kumsomesha Halima katika shule ya sekondari ya Korogwe, huku Halima Likutu akimsikiliza kwa makini .


Meneja Uhusiano wa Benki ya Posta Bi. Noves Moses akimakabidhi Vifaa vya Shule Halima Likutu ambaye baba alikuwa ameshachukua mahari kwa nia ya kumwoza huku akiwa bado mwanafunzi, darasa la saba. Mwaka jana Halima alichaguliwa kujiunga sekondari, kwa kufadhiliwa na benki hiyo.


Mtoto Halima Likutu mwenye umri wa miaka 14, mkazi wa kidatu Kilombnelo katika Mkoa wa Morogoro, ambaye alikuwa akisoma darasa la saba mwaka jana, wazazi wake walitaka kumwozesha huku wakijua kwamba umri wake ni mdogo na bado alikuwa aikoma shule ya msingi.Wazazi wake walitaka kumwozesha kiasi cha kuwa tayari walikuwa wamesha chua mahari toka kwa mwanaume ambaye jina lake tunalihifadhi zaidi kwa ajili ya upelelzi, baada ya Halima kubaini hivyo alikimbia nyumbani na kuwa kila sikumalikuwa akishinda mashambani huko Kidatu.Baada ya kuona hivyo alimwambia rafiki yake mpenzzi kuwa mimi naenda Dar es Salaam, ila akakumbuka kumwachia namba ya simu kama matokeo ya mtihani yakitoka iwapo atakuwa amefauru ampigie simu.Baada ya kufika dar es Salaam, kwa rafiki yake mama yake Pugu,Faraja Dihenga, alimwelezea mataizo aliyokuwa nayoMama huyo na Halima waliamua kwenda Redio one katika kipindi cha Kumepambazuka ambapo alipata fursa ya kuzungumzia matatizo yake, tarehe 26,Januari 2009. kinachozungumzia mazingira hatalishi.Kupitia kipindi hicho Benki ya posta imeamua kumsomesha ambapo tayari kwa kipindi chote cha maisha yake, ambapo amechaguliwa kujiunga na shure ya sekondari ya Korogwe Mkoani Tanga, tayari benki ya posta wamesha mlipia anda ya mwaka mmoja shilingi 150000, na kufungulia account yenye namba 00-00224539, tayari posta wamemwekea kiasi cha 150000.

3 comments:

Anonymous said...

MUNGU awabariki sana kwa moyo wenu wa huruma wa kumsaidia mtoto huyi. Binafsi nilisikia mahojiano katika kipindi hicho na niliumia sana roho ila uwezo sikuwa nao wa kumsaidia mtoto huyo, MUNGU awabariki sana.

Anonymous said...

Inasikitisha sana kuona hivyo ila Mungu hamtupi mja wake. Benki ya Posta Mungu awabariki.

Anonymous said...

huyu ni kumsaidia akishagraduate unamuoa wewe. huyo mshkaji aliyetaka kumharibia maisha yake anaondoka patupu, haoni ndani!!!