
Pwani Raha ilimtembelea Bw. Sylvester Lubala ambaye ni Katibu mkuu wa Tanzania Legion Club hapo jana ofisini kwake. Kwa maoni bw. Lubala alisema kuwa ni sawa yule Mkuu wa Wilaya kuwachapa wale waalimu viboko, maana alisema zamani viboko vilikuwa kama changamoto kwa watu kufanya kazi kwa bidii. Mzee huyu anakumbuka kuwa zamani Mkoa wa Shinyanga kila kaya ilikuwa imegawiwa hekari mbili za eneo la pamba na kulikuwa na uzembe uliosababisha zao hilo kudorora. Lakini uongozi uliposema kwamba watu ambao hawatalima mashamba yao watachapwa viboko, basi mashamba yao yakaanza kushawi.

Naye Ernest Binna Katibu msaidizi wa Tanzania Legion Club alipinga vikali kuchapwa kwa waalimu hao. Alisema kitendo hicho ni cha kuwadhalilisha sana waalimu. Akaongeza kuwa waalimu hawalipwi vizuri na serikali na pia fani ya ualimu imeshuka heshima yake na sio kama zamani. Bw Binna akatetea kufeli kwa wanafunzi ni kwa sababu ya mitaala mibovu ya kufundishia, utunzi wa vitabu pia hauzingatii mitaala. Alisema matokeo hayo mabovu yametokana na mgomo wa waalimu wa mwaka jana.
3 comments:
Hata mimi naunga mkono kwa walimu kuchapwa viboko was the right action taken. Kwani walimu ndio wanao sababisha kudorora kwa elimu katika wilaya zao. They deserve what they got and it should be a lesson to note for other teachers that they should be in school on time to start their lesson and not indulge into other activities.
sio njia nzuri na pia sio suluhisho, mkuu wa wilaya angekuwa mbunifu na sio kupiga watu.
It is against human rights, I do not concur with fact of punishing teachers like kids. Infact I dont like even the kids to be punished in that manner.
Post a Comment