Hapa Vivian Stephane akipokea zawadi kutoka kwa mmoja wa viongozi wa Kampuni ya Bia Tanzania.
Malikia wa Sebene wa 2007 Ketura Kihongosi akimvisha krauni Vivian Stephano ambaye aliibuka mshindi wa Malikia wa Sebene 2009 mashandano haya yalifanyika katika ukumbi wa Msasani Club Dar es Salaam, mshindi huyo wa kwanza alijinyakuliakitita cha shilingi 1,600,000. na mshindi wa pili alizawadiwa 1,400,000. Kweli global economic deterioration (recesion) haijafika Bongo.
Washiriki walioingia tano bora wa Malikia wa Sebene 2009 wakiwa katika picha ya pamoja,(kutoka kulia) Florida Gabliel , Happy Kambona, Cecilia Joseph, Sikuzani Daudi na Vivian Stephano, wakiwa wameshikilia maua baada ya kukabiziwa kama zawadi.
Washiriki wa Malikia wa Sebene wakichuana kumtafuta mshindi, usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Msasani Club.
Baadhi ya washiriki wa Malikia wa Sebene mwaka 2009 wakichuana katika hatua ya kwanza katika ukumbi wa Msasani Club. Mashindano hayo yaliandaliwa na Kampuni ya Tan Vision ya Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment