Kundi la Survival Sister ambalo linaundwa na akinadada watatu ambao ni walemavu Irene Malekala, Latifa Abdallah na Lucy Samson linatarajia kuitangaza albam yao ya Yatima ambayo ni album yao ya kwanza tangu kuanzishwa kwa kundi hilo. Akiongea katika mahojiano yaliyofanyika katika uwanja wa taifa wakati wasanii hao walipofika kushuhudi mchezo wa simba na URA ya Uganda,Irene alisema jamii inapaswa kutuunga mkono kwa kutusaidia kimawazo na kifedha,
Kikundi hicho kilianzishwa mnamo mwaka 2004 kipindi ambacho wasanii hao walikuwa wakisoma katika shule ya sekondari ya Jangwani, likijulikana kama QUEEN SISTERS na baadaye kuamua kubadili jina na kujiita Survival Sisters. Kundi hili si la kwanza kuwa na wasanii walemavu yawezekana wengi watakuwa wamesahau kulikuwa na kundi moja ambalo lilitokea kuteka nyoyo za wapenzi wa muziki wa kizazi kipya mnamo miaka ya 2001 hadi 2003.Kundi hilo lilijulikana kama kundi la Mabaga Fresh hivi sasa halijulikani liko wapi na hakuna anaye fuatilia.
















No comments:
Post a Comment