Kulia ni mmoja wa madaktari wa anayeshughulika katika huduma za wagonjwa wa akili akitoa maelezo kwa mwananchi aliyefika katika maonyesho ya Muhimbili Day yanayofanyika katika hospitali hiyo ya Muhimbili. Daktari huyo alisema kuwa wagonjwa wengi wa akili wamekuwa wakiingia na visu, nyundo, misumari, na vitu vingine vinavyoweza kudhuru, hivyo ni vizuri walezi wa wagonjwa hao kuwa makini wakati wanapowapeleka hospitalini hapo. Maadhimisho hayo yalianza jana na yatamalizika kesho.
Mwanafunzi wa kidaoto cha tatu katika shule ya sekondari ya Makongo Hassan Mussa akijaribu kumchenga mwanafunzi mwenzake wa kidato cha pili Chezo Malinda wakati wa mashindano ya kombe la Mkuu wa shule Mwagas Cup, yanayozishirikisha timu za madarasa, ikiwa ni sehemu ya kutafuta vipaji vya mpira wa kikapu.
No comments:
Post a Comment