Ufadhili wa Vodacom kwa mujibu wa imekuwa ikitoa fedha kwa lengo la kukiwezesha kituo hicho kuyakabili majukumu yake. Ni kutokana na udhamini wa Vodacom ambao umewaweka vijana shuleni hapo kwa pamoja na kwa muda mrefu ili kutekeleza program zao, vijana sita sasa watajiunga na shule maalum ya soka nchini Uhispania. Vijana hao wako katika hatua za mwisho mwisho za maandalizi ya safari hiyo. “Vijana hawa, watajiunga na shule maalum ya michezo nchini Uhispania na baada ya hapo wanaweza kujiunga na timu kubwa za madaraja ya juu nchini humo ama kwingineko Ulaya” anasema.
Rwehumbiza anasema kwamba kampuni yake inajivunia mafanikio ya kituo hicho. Anasema kwamba kwamba safari ya vijana hao kwenda nchini Uhispania ni faraja kubwa kwa kampuni yake kwani mbali na kudhamini Ligi Kuu ya Vodacom,pia kampuni yake inapenda kuona maendeleo ya vijana wadogo katika soka. “Tunaamini kwamba vijana hawa ndio watakao tengeneza timu imara ya taifa, hivyo Watanzania tuwe na imani kwamba tutakuwa na timu bora ya taifa ya wakubwa siku za usoni kutokana na kuwa na nyota wengi ughaibuni,” anasema. Anasema kwamba Vodacom Tanzania, itaendelea kuidhamini shule hiyo kwani inaamini katika kukuza soka la vijana kwa manufaa timu ya taifa ya wakubwa. Kaijage anasema kutokana na mantiki hiyo, udhamini wa udhamini wa makampuni makubwa kama Vodacom ni muhimu sana katika kufanikisha majukumu hayo. “Ili kuhakikisha kwamba taifa linakuwa na timu bora ya soka, hatuna budi kuisaidia shule yetu kwa hali na mali, Watanzania wapenda soka tushirikiane na Vodacom katika kuhakikisha tunaiendesha shule yetu bila matatizo,”.
Kaijage anatoa wito kwa makampuni mbalimbali kuisaidia shule yake kwani Vodacom pekee haiwezi kuihudumia shule kwa kila kitu, kutokana na ukweli kwamba mahitaji ya kituo yanazidi kuongezeka kila kukicha,” “Tunamahitaji mengi sana ya shule, mathalani, tunahitaji chakula, ada shule ya vijana pamoja na malazi hivyo tukiiachia kila kitu Vodacom inakuwa ni ngumu sana, ninatoa wito kwa makampuni mengine nayo kujitokeza kwa wingi kutusaidia,” Hivi karibuni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera, aliipongeza Vodacom Tanzania kwa kuboresha michezo kwa ujumla hapa nchini ikiwamo mchezo wa soka. Rais Jakaya Kikwete na hivi karibuni wakati akipokea Kombe la Dunia hapa nchini aliitaka TFF kuweka kipao mbele katika kukuza soka kwa vijana.
Mathalani katika kuutambua mchango wa Vodacom kwa maendeleo ya michezo hapa nchini Naibu Waziri Bendera anasema “Kwakweli hivi sasa Ligi hii ya Vodacom inaheshimika, heshima hii inatokana na udhamini imara wa Vodacom ambao umeziondolea timu zetu matatizo mbalimbali,” Naibu Waziri huyo anasema Duniani kote timu imara za taifa huundwa na na vilabu imara vinavyoshiriki Ligi Kuu, hivyo kwa kuwa hivi sasa tuna ligi imara maana yake hata timu yetu ya taifa ni imara. Anaipongeza Vodacom kwa udhamini huo na kuyataka makampuni mengine kuiga mfano wa Vodacom Tanzania katika kukuza soka hasa kwa kuvisaidia vilabu kuhimili gharama mbalimbali za uendeshaji wa ikiwemo gharama za usafiri. Rehumbiza anasema kwamba kampuni yake mwaka huu imetenga shilingi bilioni 1.1 kuidhamini Ligi hiyo fedha ambazo ni nyingi ikilinganmishwa na msimu uliopita ambapo kampuni yake ilitoa shilingi milioni 850. Rwehumbiza anasema Vodacom Tanzania inawekeza katika michezo kwa lengo la kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya wachezaji na hivyo kulipatia taifa wawakilishi bora katika michezo mbalimbali ya kimataifa. “Vodacom itaendelea kuboresha udhamini wake mwaka hadi mwaka kama ambavyo imekuwa ikifanya kwa lengo la kuhakikisha kwamba Ligi ya Vodacom inakuwa ni miongoni mwa Ligi bora kabisa barani Afrika” Rwehumbiza anawashukuru wadau wote ikiwemo TFF, vyama vya kitaaluma vya soka, Waandishi wa Habari ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kwamba mchezo wa Soka unakua.
No comments:
Post a Comment