Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

January 26, 2009

UZINDUZI WA GAZETI LA THE FOOTBALL

Mhariri Mtendaji Jamila Abdallah wa magazeti ya Changamoto na The Football yanayomilikiwa na Kampuni ya LadyBand akimkabidhi Sister Etien msaada wa katoni za unga wa ulezi. Sister Etien ni mkuu wa kituo hicho cha kulea watoto yatima huko Msimbazi. Msaada huu ulikiwa ni sehemu ya sherehe za kuzindua Gazeti la The Football, ambayo ilikuwa ni tarehe Januari 26 mwaka huu.
kutoka kushoto ni Mhariri wa The Football Mawazo Lusonzo, Jamilah Abdallah ambaye ni Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Changamoto na The Football, akifuatiwa na kocha mkuu wa timu ya Taifa Stars Marcio Maximo, wakala wa magazeti hayo Juma Mnete, na mhariri wa makala wa magazeti yote mawili Emmanuel Marima, wakiwa katika mpicha ya pamoja baada ya kuzindua gazeti la The Football katika ukumbi wa New Africa Hotel.

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Kanali Msataafu Idd Kipingu katikati akizindua Gazeti la The Football katika sherehe za kutimiza mwaka mmoja wa gazeti hilo katika ukumbi wa Hoteli ya New Afrika jiji Dar es Salaam, kushoto ni Mhariri mtendaji Jamilah Abdallah, Mhariri wa gazeti hilo Mawazo Lusonzo, kulia kabisa ni Makwaia Wa Kuhenga ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha Je!Tutafika? kinachorushwa na CHANEL TEN.


Mmoja wa wafanyakazi ya kulea watoto yatima katika kituo cha Msimbazi Daniela Baer akimbembeleza mtoto Noela ambaye ni miongoni mwa watoto 45 wanaolelewa katika kituo hicho kilichopo Dar es Salaam.

1 comment:

Anonymous said...

Hongera the football.