Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

August 30, 2010

Watoto wa Mitaani na Wanasiasa.



Umoja wa watoto na vijana waishio mitaani jijini Dar es Salaam, unaojulikana kama (New Hope Family Street Children-NFSC) umewataka viongozi wa vyama vya siasa wanaogombea nafasi za Urais,Ubunge na Udiwani kuwakumbuka huko wanako omba kura za kuchaguliwa. Akiongea na mratibu na afisa uhusiano wa NFSC, Andrew Chale alisema kuwa umefika wakati wa viongozi hao kuongelea machungu wanayowasibu watoto na vijana waishio katika mazingira magumu pindi wawapo katika majukwaa yao ili wananchi wapate muamko wa kuwajali. Andrew alisema kuwa wanasiasa katika kampeni zao wameshindwa kabisa kuwakumbuka hususani jamii iliyokatika mazingira magumu ikiwemo ile ya ombaomba mitaani pamoja na vijana na watoto wadogo ambapo siku zote wapo katika taabu za maisha na wanasiasa hao kuongelea maswala mengine.  “Wanasiasa wengi kipindi hichi wamesahau wajibu wa jamii iliyo katika mazingira magumu wakiwemo watoto wa mitaani hivyo tunatoa rai yetu kuwa watukumbuke sehemu zote wanazozunguka ilikuweza kusaidiwa’ alisema Andrew.

Kwa upande wake Mjumbe wa NFSC, ambaye pia ni Mwanaharakati wa kutetea Haki za Watoto Nchini na Mwenyekiti wa Chipukizi Wilaya ya Kinondoni, Nimka  Lameck (10) alitoa wito kwa jamii kuwa na moyo wa huruma ikiwemo kuchagua viongozi watakao jari maslai kwa  watoto wakiwemo wale wa mitaani na waliokatika manyanyaso kwenye familia.  “Umefika wakati wananchi kuchukua hatua za haraka ikiwemo kwa viongozi ambao wanashindwa kutetea haki zetu sisi watoto pamoja na jamii iliyo masikini kwa kuwakataa na kutiowachagua” alisema Nimka. Aidha, NFSC pia ilitoa wito kwa jamii kuendelea kujitokeza kuwasaidia michango mbalimbali ikiwemo ya fedha na vitu ilikujikimu katika maisha. “Mpaka sasa tumefanikiwa kupata nyumba ya kupanga huko Kigamboni ambapo tunatalajiwa kulipia Milioni moja na laki mbili hivyo tunaomba msaada wa haraka ikiwemo magodoro,vitanda na vyombo vya ndani’ alisema Andrew.

New Hope Family Street Children-NFSC, unajumuisha vijana na watoto waishio katika mazingira magumu na hatarishi katikati ya jiji la Dar es Salaam ipo chini ya Mwenyekiti  Omary Rajabu na Katibu wake Hashimu Yusuph. Kwa mtu aliye na mchango wa haraka anaomba kuiwakilisha katika ofisi za gazeti ili zilizopo mtaa wa mkwepu jengo la Billicanas na kuonana na Deodatu Mkuchu 0756090483/ Andrew 0719076376. 

No comments: