Poleni sana kwa majukumu mazito ya kazi yanayayowakabili. Naimani kuwa sote tuwazima na Mungu anazidi kutupa nguvu ya kuutumikia umma. Aprili 30, 2010 nilipokea ujumbe kutoka kwa ndugu yetu Athuman Hamisi Msengi ambaye alipata ajali 2008 mwishoni na kupelekwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi. Athumani amekuwa Nchini Afrika Kusini kwa muda mrefu na tunawashukuru wale ambao walikuwa wakipata nafasi ya kwenda nchini humo kwa shughuli za kikazi au binafsi na kupata fursa ya kumtembelea na kumjulia hali na kumfanya ajisikie yupo nyumbani. Athumani ameniambia kuwa anataraji kurejea nyumbani Mei 8, 2010 saa 12 jioni, South African Airways hivyo tujitokeze kwa wingi kadri ya nafasi zetu kumpokea na kumkaribisha nyumbani ndugu yetu. Ni imani yangu kuwa wengi wetu tutakuwepo na kushirikiana katika hilo. Ufuatao ni Ujumbe kutoka kwa Athumani:- "Salaam, Safari imeiva. Narudi Tanzania Mei 8, saa 12 jioni. Msisikitike kuniona ktk wheelchair, mikono na miguu haifanyi kazi. Nikazi ya Mungu haina makosa." "Natanguliza shukrani na kuwatakia kazi njema. NB Ukipata Ujumbe huu mtaarifu na mwenzako maana si wote wafunguao barua pepe zao.



















No comments:
Post a Comment