Mkuu wa Wilaya ya Lindi ya mkoa wa lindi.Magalula Said akipokea msaada wa komputa 20 zenyethamani ya shilingi Milioni 15 kutoka kwa Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba (kulia) kushoto ni wanafunzi wa shule ya sekomdari ya Mnolela wakishuhudia msaada huo uliotolewa kwa shule mbili za mnolele na Mtama, mpaka sasa kitengo cha Vodacom Foundation ambacho ndicho kinachoshughulika na utoaji wa misaada mbalilmabli katika jamii ya watanzania mbaka sasa kimesha tumia kiasi cha shilingi Mbilioni 3 katika kuhudumia wananchi wa Tanzania .

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mnolela iliyopo kata ya Ruhokwa katika Wilaya ya Lindi wakiangalia picha za sherehe yao ya kukabidhiwa msaada wa komputa baada ya kuwa tayari zimewekwa katika mtandao , Vodacom Tanzania walitoa msaada wa komputa 10 zilizounganishwa na Intarnet zikiwa na gharama ya shilingi Milioni 7.5

Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom Mwamvita Makamba akiwaonyesha wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mnolela namna ya kutumia komputa kwa njia ya Mtandao baada ya kuwakabidhi msaada huo .

Mkuu wa Wilaya ya Lindi Magalula Said akimakabidhi msaada wa komputa moja kati ya 10 walizokabidhiwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mnolela Bahia Abubakar ,baada ya Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba kulia kumkabidhi msaada huo mkuu wa wilaya ya Lindi.

VODACOM HOYEEEEEEEEEEEE,,Mnolela hoyeeeeeeeeee. Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom Mwamvita Makamba akiwa hutubia wananchi wa Ruhokwa wakati wa sherehe za kuwakabidhi msaada wa komputa 20 kwa shule za sekondari za Mnolela na Mtama.zote za wilaya ya Lindi,
No comments:
Post a Comment