Hili ni moja ya makundi yaliyoibuka washindi katika Sasatel Quiz Night iliyofanyika Peacock Hotel. Kampuni ya Sasatel iliandaa mashindano ya kujibu maswali ijumaa iliyopita ambapo mlango ulikuwa wazi wa mtu yoyote kushiriki. Kiingilio kilikuwa bure lakini kinyume na matarajio ya wengi mshiriki alikuwa anajilipia mwenyewe kinywaji na chakula jambo ambalo halikuwekwa wazi wakati wa matangazo yao ya kuvutia washiriki. "vinywaji na chakula bei ndege, mwisho wa siku ukiangalia zawadi na hela uliyotumia ni hasara tupu" alisikika akilalamika mmoja ya washiriki.
December 10, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment