Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

November 10, 2009

Likonde Mtwara

kutoka kulia ni kijana mwenye umri wa miaka 18 Ali Juma aliyemaliza darasa la saba katika shule ya msingi ya Likonde Mtwara, akiwafundisha watoto Tounguen Mfaume mwenye miaka 12 katikati na Mloka Mniba mwenye umri wa miaka 7 namna ya kubambua korosho. Watoto wengi wenye umri mdogo wa kwenda shule wamekuwa wakishindwa kwenda shule kutokana na ukata wa kimaisha na kuamua kujikita katika shughuli za ubambuaji wa korosho.



Ali Juma akiwa kazini, kazi hii ya ubanguaji wa korosho aliianza tangua mwaka 2008 ambapo alikuwa darasa la sita. Mpaka sasa ameweza kununua fenicha za ndani kama vile kitanda n.k. Ali amemaliza darasa la saba mwaka huu lakini anasema hana uhakika wa kuendelea na masomo kutokana na ukata wa fedha kwani hata shule ya msingi amesomeshwa na kikundi cha Nyerere youth Development ambacho kimekuwa na mchakato wa kujitolea na kuwasaidia watoto waishio katika mazingira magumu.


Kundi hilo limeamua kuanzisha huduma za kufanya usafi katika halmashauri ya mtwata mjini hivyo kila kaya hulazimika kulipa shilingi 200 kwa kila siku na pesa zinazopatikana ndizo zinazowasomesha watoto hawa waliofiwa na baadhi ya wazazi. Mpaka sasa tayari kikundi hicho kinawasomesha watoto 31, wawili wakiwa wamejiunga na shule ya sekondari.


Adha ya maji si Dar es Salaam tu ni tatizo la nchi nzima, akinamama wa Likonde Mtwara wakiwa katika foleni ya kusuburi kuchota maji katika kisima cha idara ya maji ya Mtwara.

No comments: