
Wachezaji wa Simba wakifanya mazoezi katika uwanja wa Uhuru kabla ya kuanza mtanange na Jkt Ruvu wakiwa wamesimamiwa na Meneja msaidizi wa klabu hiyo Amri Said katika mchezo huo uliofanyika jana jioni Simba iliwararua maafande wa Kujenga Taifa, JKT 4-1.

Rais wa shirika la mpira Tanzania (TFF) Bw. Tenga akibadilishana mawazo na kocha mkuu wa Timu ya taifa Macio Maximo kabla ya kuanza mchezo wa Simba na JKT.

Kocha mkuu wa Simba aliyesimama Patrick Phiri , Innocenti Njovu na Amri said wakishuhudia Simba inavyotoa kipigo cha magoli 4-1

Hapa ndipo ngoma inogile wanenguaji wa bendi ya FM Acadenia wazee wa pamba ,Aliya Ronardinho kushoto na Lili Mkwajuni wakiwapagawisha mashabiki wa bendi hiyo jana usiku katika ukumbi wa New Msasani Klabu.
No comments:
Post a Comment