Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

October 6, 2009

Mlemavu wa Macho Aliza Wanawake Wenzake.

Mmoja wa akina mama ambaye ni mlemavu wa macho( asiye ona) Rehema Darushi ambaye ni mwalimu shule ya wasiona katika shule ya Tuangoma ya Kigamboni na Shule ya Msingi Kibasila akieleza jinsi alivyojifungua watoto mapacha katika hospitali ya Muhimbili na pamoja alivyoaibiwa na manesi mbele ya Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii David Mwakyusa hayupo pichani wakati wa kongamano la jukwaaa la pili la wazi juu ya maisha ya wanawake na wasichana lililofanyika leo katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam. Likiwa limeandaliwa na TAMWA kushoto ni mtoto wake Salama John mwenye umri wa miaka kumi na mbili ambaye ndiye anayemsaidia katika shughuli zake za kila siku.

Baadhi ya akina mama waliohudhuria katika kongamano la Jukwaa la pili la wazi juu ya maisha ya wasichana na wanawake na ukweli kuhusu vifo vitokanavyo na uzazi na ulemavu.

Balozi wa Uingereza hapa nchini Diana Coner kulia na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii David Mwakyusa wakimsikiliza kwa makaini Mwalimu wa shule ya msingi Kibasila anayefundisha watoto wasioona Rehema Darushi hayupo pichani wakati alipokuwa akielezea jinsi alivyojifungua watoto mapacha katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na njisi manesi walivyo mwiba mtoto huyo na kumdanganya kuwa alijifungu mtoto mmoja lakini wakati huo huo alikuwa amefungwa kamba 2 kama ishara ya kujifungua watoto wawili Rehema ni mlemavu wa macho haouni lakini wenzake walikuwa wakimsifia kuwa kajifungua watoto wazuri mapacha, hivyo waziri wa afya ametoa jibu kuwa watu wengi wanapoteza haki zao katika hospitali hiyo kwa kushindwa kufikisha madai yao sehemu husika na amewaahidi wananchi watakaopata shida yeyote ikiwemo ya rushwa wafike moja kwa moja kwake.


Kutoka kushoto Sikudhani Ahmad akifuatiwa na bibi yake Jene Lugema, mamayake Mwajuma Bakari na mamayake mdogo Mary Hamisi wakiwa wamepozi nyumbani kwao Kinondoni jijini Dar es salaam.

No comments: