Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

September 18, 2009

Msondo yawanasa Wanamuziki Wapya.

Kutoka mkushoto Juma Katunda akizungumuza na wandishi wa habari wakati wa mkutano wa utambulisho wao wa kujiunga na bendi ya Msondo uliyofanyika katika ukumbi wa Amana. (katikati) Edmund Sanga na Mkurugenzi wa bendi hiyo Muhidini Ngurumo. Bendi hiyo inatarajia kuzindua albamu yao mpya itakayojulikana kwa jina la Hana Shukurani ambayo itakuwa na nyimbo saba.
Bendi ya muziki wa dansi ya Msondo Ngoma imeiimarisha safu yake ya uimbaji kwa kuwanasa waimbaji wawili mahiri nchini, Rashid Mwezingo na Edo Sanga. Akizungumza kwenye ukumbi wa Amana jana, kiongozi wa bendi hiyo, Muhidin Maalimu Gurumo alisema kuwa wameamua kuwachukua wanamuziki hao ili kujenga safu imara ya uimbaji. Mwezingo maarufu kama Silver Boy, amejipatia heshima katika fani ya muziki wa dansi kutokana na uwezo mkubwa aliounyesha alipokuwa na bendi za Mchinga Sound, Double Extra, African Revolution 'Wana Tam Tam' na TOT Plus.
.
Edo Sanga ni kama anarudi nyumbani baada ya kuihama bendi hiyo mwaka jana na kujiunga na DDC Mlimani Park 'Sikinde Ngoma ya Ukae' ambayo hivi sasa inajulikana kama Orchestre Mlimani Park."Ni waimbaji wazuri na wanauwezo. Tumeona kuwa nao katika bendi yetu kutatuwezesha kuwa na safu imara zaidi ya waimbaji," alisema Gurumo.Gurumo alisema kuwa waimbaji hao wataungana na waimbaji wengine wa bendi hiyo Juma Katundu, Papa Upanga na Gurumo mwenyewe na kwamba wataanza kuitumikia bendi hiyo wakati wa siku kuu ya Idd katika ukumbi wa Amana."Idd Mosi tutaanza kufanya maonyesho katika ukumbi wetu wa zamani wa Amana Club Ilala na wapenzi wa muziki wataanza kuwashuhudia kwa mara ya kwanza bendi hii ikiwaatumia wanamuziki hawa,"
.
Wakati huo huo Gurumo aliwapongeza wandishi wa habari nchini hasa ware wanaoandika burudani kwa kwenda na wakati na kuahidi kuwatungia wimbo utawa kuwapongeza kitendo hicho kinatokana na utovu wanidhamu unaonyeshwa na wanataaruma ya uandishi kwa wananchi.
.
Naye kiongozi wa bendi hiyo Said Mabala aliwambia wandishi wa habari kuwa mpaka sasa bendi ya Msondo Ngoma tiyari ina albamu mbili ambazo alizitaja kwa jina la Hunashukrani na Kicheko, albamu mpya ambayo inategemewa kuzinduliwa mwezi Oktoba mwishoni.
Albamu hiyo tayari imesha kamilika na inanyimbo saba ambazo Gurumo alizitaja kuwa ni Huna shukurani uliotungwa na Said Mabela,Cheo ni dhamana wa Eda Sanga,Kiapo ambao umetungwa na Husein Jumbe nyingine ni Mema kosi wa Maina ,Maalbaino ambao umetungwa na wanamuziki wote wa Msondo,Urithi uliotungwa na Gurumo na wamwisho unajulikana kwa jina la Kimya kingi uliotungwa na Papa Upanga.

Kiongozi wa bendi ya Msondo Baba wa Muziki Said Mabela akiwa katika pozi wakati wa mkutano na wandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Amana Jijini Dar es Salaam, ambao ulikuwa na lengo la kuwatambulisha wanamuziki wapya waliojiunga na bendi hiyo kongwe.

Muhidini Ngurumo ambaye ni Mkurugrugenzi na kiongozi mkuu wa bendi ya Msondo.

No comments: