
Msajili wa vyama vya siasa John Tendwa akitoa ufafanuzi kuhusiana na tume ya uchanguzi wakatimalipokuwa akihutubia wanachama wa CUF katika viwanja vya Kidongo Chekundu Dar es Salaam

Msajili wa Vyama vya siasa Vicent Tendwa kulia akimweleza jambo Mwenyekiti wa chama cha Cuf Ibrahim Lipumba wakati walipokuwa katika viwanja vya Kidongo chekundu ambapo chama cha wananchi cuf kilifanyia mkutano wa kuitaka tume ya uchaguzi ijiuzuru.

umati wa watu walioandamana wakiitaka tume ya uchaguzi ijiuzuru wakiwa katika maeneo ya barabara ya uhuru,maandamano hayo yaliandaliwa na Cuf na kuwashirikisha wananchi wote wenye uchungu na nchi yao yalianzia katika ofisi za Cuf Buguruni na kuishia katika viwanja vya Kidongo chekundu.

Askali polisi wakiwa wamezuia maandamono katika makutano ya barabara ya uhuru na bibi titi mohamed mnazi mmoja.

Baadhi ya wanachama wakiwataka askari waruhusu maandamano yafike katika ofisi za msajili wa Vyama ,hata hivyo maandamno hayo yameishia katika viwanja vya kidongo chekundu.
Picha zaidi.....

Mwanachama mkerereketwa wa Cuf akikokota pikipiki yake baada ya kuzimika akiwa katika msafala wa maandamano yaliyoandaliwa na cuf kwa niaba ya kuishinikiza tume ya uchaguzi ijiuzulu.

akina mama kwa akina baba wakiwa kwenye bajaji huku wakiwa na bendera za Cuf wakati wa maandamano ya kuitaka tume ya uchaguzi ijiuzuru.maandamano hayo yalishia katika viwanja vya Kidongo chekundu
No comments:
Post a Comment