Pages

September 17, 2009

Baba Mkwe Mpiga Picha Mkuu Mazishini

Mmzee Hamis Chifupa akiwa bize na kupiga picha marehemu Mohamed Kheri Mpakanjia wakati akiswaliwa katika msikiti jijini Dar es Salaam, watu wengi walishikwa na butwa kwa mzee huyo kuwa bize kiasi hicho badara ya kuwa na majonzi.


Baba mkwe wa marehemu Mohamed kheri Mpakanjia aliyefariki juzi na kuzikwa katika makaburi ya kisutu,anakuwa bize na kupiga picha za marehemu.

6 comments:

  1. Pamoja na yote MTU huwezi kulazimisha majonzi wala kulazimishwa uwe na Majonzi ingawa mila na desturi zetu zinamchezo wakutaka kufanya huo ndio uwe uhalisia.


    Na kila mtu anastaili zake za kusononeka na majonzi.

    Kuna watu wanalia kirahisi kwa nguvu zote mara moja yanaisha na kuna watu wanalia kila siku kiadoado na unaweza usistukia waliliacho ni miaka tayari imepita na bado wako katika majonzi.

    Lakini pia hakuna sehemu zenye wanafiki wengi kama misibani ambako mpaka maadui wa marehemu utawasikia wanadai:''Marehemu alikuwa mtu mzuri !'':-(

    ReplyDelete
  2. Inawezekana mzee Alipitwa na picha za maziko ya binti yake.kwahiyo alihakikisha hakosi picha hapa.

    ReplyDelete
  3. Ni kweli usemayo Simon.

    ReplyDelete
  4. Anonymous3:11 PM

    Hata wewe uliempiga picha mzee Chifupa ni mnafiki flani vile, kwamtazamo wako unadhani mzee wa watu hana majonzi kwa kupiga picha za matukio ya msiba kwa kigezo kipi? hata wewe vilivile ulikwenda kuchunguza watu na wala hukuwa na majonzi ndio maana unatundika upuuzi huu jamvini - ACHA HIZO!

    ReplyDelete
  5. Anonymous6:53 PM

    Kila mtu ana haki ya kutoa mawazo yake, hayo ni mawazo yako anony hapo juu.

    ReplyDelete
  6. Anonymous7:43 PM

    Majonzi alokua nayo, wakati wa msiba wa mwanae yanatosha!, wacha alambe picha za msiba wa aliekua mkwewe!, kwanaza kulikua mushkeri kuhusu kifo cha Kifupa Meddy kamfuata mkewe RIP.

    ReplyDelete