Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

August 7, 2009

Royal Prince Saloon Sinza Wako Juu. (Men Hair Saloon in Tanzania)

Katika jambo ambalo Dar es salaam linajitahidi ni kuwa saloon za kiume zilizo za ukweli, tafauti na zamani mteja akienda kunyoa nywele mpaka aende akaoge. Katika eneo la Sinza Pwani Raha imevutiwa na saloon ya Royal Prince jinsi walivyowasafi, huduma pamoja na vifaa.


Kwanza kabisa sehemu inaeneo zuri la kuegesha magari kwa wateja, pili saloon yenyewe ina mvuto unaoonekana kwa nje.

Hii ni madhari ya ndani ya saloon full kipukwe "air conditioned" hapa mteja anapewa huduma ya hali ya juu.

Hapa Abul Ramadhani akimnyoa ndevu mteja kwakutumia "magic".

Ismail Kakusa 28 akimfanyia scrub mteja. Ismail ni kinyozi mwenye uzoefu mkubwa kiasi kwamba ameweza kupata mafanikio makubwa binafsi hadi kujenga nyumba yake mwenyewe iliyoko Tabata Bima hapa Dar es salaam kutokana na shughuli hii. Kwa stori zaidi...... bonyezi neno "zaidi".

Mteja akiwekwa kwenye mashine ya kunyonya mafuta usoni baada ya kufanyiwa scrub.

Denyo Moses akionyesha jinsi vifaa vya kunyelewa vinavyohifadhiwa sehemu nzuri na kwa usafi.

Mteja anapomaliza kunyolewa, huoshwa katika sehemu hii maalum.

Kwa kina adada na kina kaka wenye kufanya pedique na manique basi hii ndio sehemu yake.

Baadhi ya vinyozi wa Royal Prince wakipiga picha ya pamoja.



5 comments:

Anonymous said...

Muko juu nimekubali ni changamoto kwa wengine.

Nicky Mwangoka said...

Kumbe kuna kiwanja cha nguvu hivyo hapo, lazima niwahi nikaongeze "uhandsome".Shukrani kwa kuwasilisha.

Anonymous said...

Saloon safi, ila itakuwa bei kubwa mimi hunyoa chini ya mwembe lakini matokeo ni sawa sawa. Yani hakuna anayeweza kutambua kama nimenyolewa wapi. Kinyozi wangu noma sana. Uchumi unakaba ndo maana hatuonekani huko.

Anonymous said...

Sidhina kama ni ghali. mbona kawaida sana.

Anonymous said...

maendeleo nimeona kwenye picha na vyombo munavyo lakini huduma inayotolewa sijaona swali langu je mnapaka rangi nywele -kusuka- massage -design.