Asubuhi hi madereva wa mabasi yaendayo mikoani wamegoma. Tangu alfajiri leo asubuhi hakuna basi lolote lililotoka Ubungo bus Terminal. Madereva hawa wanadai kwamba dereva mwenzao alikuwa akiendesha mabasi ya Mohamed Trans aachiwe huru. Dereva huyu alihukumiwa kwenda miaka thelathini jela baada ya kusababisha ajali iliyoua mtu. Madereva hao wanasema kuwa ball joint ya basi hilo ilichomoka na kusababisha basi kupoteza mwelekeo hatimaye kusababisha ajali hiyo.
Hadi hivi sasa Hakuna basi lolote lililondoka Ubungo isipokuwa mabasi mawili ya Tahmeed ambayo huwa hayaingii kituoni Ubungo. Safari yake uanzia Kariakoo (Lumumba) na kuenda moja kwa moja hadi Tanga au Mombasa.
August 14, 2009
Madereva Ubungo Wagoma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

3 comments:
Kamanda Kova ndio amefika sasa hivi, wanaendelea na mazungumzo. Naona hapa FFU wapo maana kuna madereva fulani walitaka kuanza safari hapo awali matokeo yake wakala kichapo na madereva wanzao.
Kamanda Kova ndio amefika sasa hivi, wanaendelea na mazungumzo. Naona hapa FFU wapo maana kuna madereva fulani walitaka kuanza safari hapo awali matokeo yake wakala kichapo na madereva wanzao.
Mizengo Pinda ameshatatua tatizo magari yameanza safari kuelekea mikoani.
Post a Comment