
Mbunge wa CCM wa jimbo la Bariadi Mashariki , Mh, Andrew Chenge majira ya saa 10 alfajiri kuamkia leo amepata ajali ya gari alilokuwa akiendesha aina ya Totota Hillux lenye namba za usajili T512ACE katika maeneo ya makutano ya barabara za Haillesalasie na Karume eneo la Oysterbay jijini.

Gari la Mh Chenge liligonga Bajaj yenye namba za usajili T736AHC na kusababisha vifo vya watu wawili ambao walikuwa abiria katika bajaj hiyo.

Hii hapa ni insurance ya gari la Mh Chenge, kwa muonekano inaonyesha kuwa imeisha mwaka juzi tarehe 6 Mwezi wa Aprili 2007. Sasa sijui sheria zinasemaje ukiwa umegonga na hauna insurance.

Damu iliyoganda kwenye gari la Mheshimiwa.

Chenge alikuwa akitokea maeneo ya St Peter na dereva wa bajaj alikuwa ikitokea katika ukumbi wa maisha klabu iliyopo pia oysterbay, chenge ambaye kwa sasa anashikiriwa katika mkituo cha polisi cha oysterbay wakati akihojiwa na maafisa wa jeshi la polisi wakiongozwa na Naibu Kamishina wa makosa ya Jinai DCI Peter Kivuyo alisema kuwa chanzo cha ajari ni dereva wa bajaj alijalibu kuovateki magari.

Naye mmoja wa ndugu wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la January Constantine akisema kuwa mmoja wa marehe ni dada yake ambaye alimtaja kwa jina la Beatrice Costantine mwenye umri wa miaka 38,ambaye ni mkazi wa mwanza aliuja juzi Dar es Salaam, kwa ajili ya kwenda Zanzaibar kufuata biashara ya Vitambaa ambayo ndiyo shughuli yake ya kila siku,pia aliendelea kwa kusema tukio hilo lilitokea wao wakiwa safarini kuekekea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jk Nyerere wakijandaa kuelekea Zanzaibar ambapo mwenzake alitegemea kufunga.

Chenge akiwa Polisi Oysterbay.
4 comments:
Nimeshangaa kuona kuwa pamoja na vifo vilivyotokea hapo, watu wanatabasamu kama vile wako kwenye sherehe. Na watoto nao wako hapo, na inaonekana ni sawa tu. Enzi za mababu na mabibi, kulikuwa na miiko. Nchi imekwisha.
Hata mimi nashangaa sana, insurance yake imekwisha.
huyo ni mpuuzi tu,alikidharau kibajaji ndio maana akakigonga,yeye si ana ma bilion ughaibuni kayachimbia huko,mali ya umma..
ashikishwe adabu mshenzi huyo...halafu na nyie mnaochangia hii maada,kama watoto zenu au dada zenu ndo wagengongwa na chenge,mngesema asamehewe?acheni ujinga wenu,au kwa vile chenge ni kigogo nini ndio umnamshobokea? hiyo ni moja wapo ya laana na mabalaa ya kuiba mali za walala hoi wa nchi hii...
msnhenzi huyu nina hasira nae sana..sheria ichukue mkondo wake..fisadi mkubwa yule..
Sasa sijui kama ataepuka vipi hii issue ya insurance I want to know sheria inasemaje kuhusu insurance kuisha na wakati kagonga.
Post a Comment