Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

February 19, 2009

NOKIA WAANZISHA KAMPENI YA KUKUSANYA SIMU ZA ZAMANI (SIMU ZISIZOTUMIKA)

Dorothy Ooko , Communication Manager, East and Southern Africa wa Nokia akiongea na waandishi wa habari.


Nick Maina, Customer Care Manager Nokia East Africa.

Waandishi wa habari wakisikiza kwa makini alichokuwa anasema Nick Maina kuhusu utafiti wa Nokia.

Jinsi simu mbovu zinaweza kukusanywa na kutumika kwa manufaa ya jamii.

Nick maina kushoto akishikilia boxi la nokia litakalotumika kukusanya simu mbovu na huku Dorothy Ooko akitumbutiza simu mbovu.

Mkereketwa akiweka simu yake ya zamani baada ya kupata somo.
Wengi hawajui kama simu za zamani zinaweza kutumika kutengeneza vitu vingine- Utafiti wa NOKIA.
.
UTAFITI kuhusu matumizi ya simu duniani uliofanywa na Kampuni Kubwa ya simu za mkononi Duniani-NOKIA, umeonyesha kuwa ni asilimia 3 tu ya watu wana fahamu kuwa simu zao za zamani zinaweza kurudishwa na kutumika kutengenezea vitu vingine (recycle) pamoja na ukweli kwamba wengi wao wana simu za zamani na hawazitumii tena.
.
Kwa mujibu wa utafiti wa NOKIA, watu watatu kati ya wanne duniani hawafikirii kabisa ku-recycle simu zao huku karibu ya nusu yao hata hawajui kama inawezekana ku-recycle simu zilizotumika.
Utafiti wa NOKIA ulihusisha kuwahoji watu 6,500 katika nchi 13 duniani ikiwamo Nigeria ambayo iliwakisha soko la Afrika. Utafiti huo ulifanywa na NOKIA ili kujua mwenendo wa wateja wa simu kuhusu kurecycle ili kuusaidia mpango wa kampuni hii wa kurudisha simu zilizotumika na kuongeza kiwango cha kuzirecycle simu za zamani.
.
Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo watumiaji wake wengi hawafahamu kama inawezekana ku-recycle simu zilizotumika kitu ambacho kinaendana na matokeo ya utafiti wa NOKIA.
.
“Watu wengi hawajui kama simu hizi zinaweza kuwa re-cycled. Na wengi hawajui namna ya kufanya re-cycling. Nokia inamrahisishia mteja kwa kumpa taarifa kupitia mpango wetu wa Kurudisha Simu kama huu tunaoushuhudia leo. Tunataka kila mtu atambue wapi ataweza kupeleka simu zake za zamani,” alisema Nicholas Maina, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa NOKIA Kanda ya Afrika Mashariki.
..
Utafiti umeonyesha kuwa kama kila mtu kati ya watu bilioni 3 wanaomiliki simu wangerudisha simu angalau moja tu, itakuwa sawa na kuokoa tani 240,000 za malighafi ya kutengenezea simu na hivyo kupunguza athari za kimazingira hasa mabadiliko ya hewa. Malighafi tani 240,00 ni sawa na kuyaondoa barabarani magari milioni 4 ambayo yanatoa hewa chafu inayoathiri mazingira.
.
Matokeo ya utafiti yanaonyesha pia kuwa pamoja na watu wengi kuwa waliwahi kumiliki wastani wa simu tano, chache sana zinakuwa re-cycled zinapokuwa hazihitajiki. Ni asilimia 3 tu ndo walisema wamere-cycle simu zao wakati asilimia 44 walisema wanazitunza nyumbani tu. Wengine walisema simu za zamani wanaziwapa ndugu na jamaa zao.
.
Dunia kote, asilimia 74 ya watumiaji wa simu waliohojiwa walisema hawafikirii ku-recycle ingawa asimia 72 walikiri kwamba kufanya hivyo kuna faida kwa mazingira kwa. Majibu hayo yalifanana karibu katika nchi zote. Maina alisema hadi kufikia asilimia 80 ya simu za NOKIA zinaweza kuwa re-cycled na baadhi ya malighafi zinaweza kutumika kutengenezea bidhaa nyingine kama vile birika za kuchemshia maji, benchi za kukalia kwenye sehemu za mapumziko, vifaa vya kuzibia meno na hata kifaa kama saxophone na vifaa vingine vya bati vya muziki.
.
Kati ya asilimia 65 na 80 ya simu moja ya zamani huweza kutumika kwa kazi nyingine na sehemu iliyobaki kama vile plastiki, hutumika kuwasha moto wa kuyeyushia sehemu za simu. Vifaa vingine hukusanywa pamoja na kubanwa na huweza kutumika katika ujenzi wa barabara au majengo. Kati ya nchi zilizofanyiwa utafiti, India iliongoza kwa kuwa na watumiaji wa simu wasiojua kama inawezekana ku-recycle simu ikiwa na asilimia 17 tu ya wanaojua, Indonesia asilimia 29 na nchi zilizokuwa na ufahamu mkubwa ni Uingereza ikiwa na asilimia 80 huku Finland na Sweden zikiwa na asilimia 66.
.
NOKIA imeandaa maeneo ya kukusanya simu ambazo hazihitajiki katika nchi 85 duniani kote, mpango ambao ni mkubwa wa kujitolea katika sekta simu ya mkononi. Kwa Tanzania wateja wa NOKIA wanaweza kupeleka simu zao za zamani ambazo hawazitumii kwenye ofisi za Authentic-Harbour View Mall zilizopo mtaa wa Samora na Midcom Service Centre bara bara ya Alihassan Mwinyi.
.
“Tunaitikia wito wa utafiti huu kwa kuendesha mfululuzo wa kampeni na shughuli za kuwahabarisha watu juu ya namna na wapi wanaweza kupeleka simu zao za zamani, chaji na vifaa vingine vidogovidogo vya simu. Pia tunaongeza idadi ya mapipa ya kukusanyia simu kwenye vituo vyetu vya huduma kwa wateja na kuzitangaza ili kuleta uelewa zaidi miongoni mwa wateja wetu. Vituo vyetu vya NOKIA pia vinahakikisha wateja wake wanapata huduma za wataalaamu wa matengenezo ya simu zao, kupata programu mpya za compyuta mpya kwa ajili ya simu na msaada wa kiufundi kwa ujumla. Vituo vya huduma kwa wateja ni sawa na vile vinavyopatikana Ulaya na Mashariki ya Kati.

1 comment:

Anonymous said...

Bongo watupe simu mbovu hilo sidhani simu huenda kwa mtindo wa kurithi, ikiisha anapewa braza au sister, then akimaliza kuitumia anatewa binamu, binamu akimaliza anapewa beki tatu, beki tatu ( house gal)naye anamuhonga boi frendi wake ambaye ni gardener, gardener huitunza sana ikitoka screw huiweka rubber bendi au bigG. bongo bado.