Jamani kuanzi tarehe moja mwezi ujao, mtu yeyote yule ambaye atataka kumlipa mwenzake kiasi cha fedha cha zaidi ya milioni kumi (10,000,000) kwa kutumia cheki ya benki moja ili mlipwaji a-depositi benki nyengine (benki yake), haitawezekana tena.
Mfano mwengine ni huu; Yani kama unamdai mtu hela kiasi cha zaidi ya milioni kumi (10,000,000) kisha huyo mtu akulipe kwa kutumia cheki basi wewe kataa maana ukiipeleka hiyo cheki katika benki yako itakataliwa. Lakini kama cheki ni chini ya milioni kumi haina tatizo.
Hii ina maana kuwa Clearing House ya Benki Kuu ya Tanzania haikubali malipo binasfi ya cheki zinazo zidi milioni kumi. Badala yake kama unataka kumlipa mtu hela zaidi ya milioni kumi basi njia ni hizi zifuatayo;
1. Mdumbukizie pesa kwenye akaunti yake kwa kuenda wewe binafsi au mwakilishi wako katika benki yake.
2. Nenda katika benki yako kisha uiagize benki yako itume hela kwa mfumo wa TISS (Tanzania Interbank Settlement System)
3. Mlipe taslimu (cash).
UFAFANUZI
1. Kama mtu amekupa cheki ya benki ambayo wewe pia una akaunti kwa jina hilo hilo lililoandikwa kwenye Cheki basi haina noma hataka kama imezidi milioni kumi italipwa tu ilimradi mlipaji awe na hela za kutosha kwenye akaunti husika.
2. Malipo yote ya Cheki ya chini ya milioni kumi hatakuwa kama kawaida.
3. Special Clearance ya zaidi ya milioni kumi itakuwa hakuna tena.
4. Malipo yote ya Cheki za Serikali yatakuwa kama kawaida.
Ikumbukwe kuwa ni malipo yale tu yanayohusisha benki mbili yani (bank to bank payments) ndio tunayoyaongelea.
6 comments:
Hivi inakuwajesema tuna rudi au mbele.
Hiyo ni one of the loophole, cheki mbili zinaweza kukubalika pengine uzipileke mida tofauti. Labda cheki moja ya 7M nyingeni 3M, ama kama unavyosema 5M then nyengine ya 5M. Lengo la BoT hawajaliweza bayana ila binafsi nadhani ni kwa sababu wizi mwingi wa Cheki. Sasa kwa ku-discourage large amounts kupita clearing house basi wizi namna hiyo utapungua. Wao wanahamasisha wateja kutumia (TISS) maana humfikia mlengwa halisi kuliko cheki ambayo ni rahisi kuwa intervened na baadaye kutomfika mlengwa halisi.
Wezi wa cheki hutumia akili nyingi na fedha nyingi pia, sasa ikiwa cheki itakuwa na amount kubwa basi haijalishi gharama watakazotumia. Ila kama Cheki ni ya milioni 9 tu basi dili hilo litakuwa sio poa yani kwa lugha nyingine (it doesnt worth the risk).
Sasa basi ninavyoona mimi hii itakuwa na athari kubwa wafanyibiashara wengine. mfano kuna watu humlipa supplier kwa Cheki kama 40M huku kwenye benki hana hela, lakini anajuwa kuwa akipata ile bidhaa ataiuza ndani ya siku mbili kisha atapeleka hela benki ili Cheki ile ikifika ikute hela zimo. Hawa ni wafanyibiashara wa first moving goods kama vile mafata (fuel). wanafanya hivyo maana Cheki huchukuwa siku 4 za kazi ili ku-mature.
bado sijaona sababu ya hatua hiyo pamoja na kutuwekea maelezo marefu. hoja ya mdau kuwa ni kupunguza wizisioni kama ina nafasi sababu njia sahihi za kudhibiti wezi au udaganyifu ni kuongeza teknolojia sio kurudi nyuma tulikotoka. jee mafisadi wanappewa 10 percent ktk miradi mikubwa ya serikali watadhibitiwa vipi?
Sababu nyengine inawezakuwa kupunguza float na ukiritimba wa mabenki chelewesha kuwalipa watu cheki zao. Float Cheti ambazo hazija mature, sasa benki yengine huongeza muda wa cheki ku-mature ili mteja asiweze kuchukua hela kwa haraka alafu Benki ipate muda mrefu wakuzitumia Hela hizo. Yani Benki ikiwa na float nyingi inakuwa vizuri kwao, wanaweza kuzitumia hizo hela kulipia cheki za inward (Cheki ambazo wateja wabenki hiyo walizolipa watu). Benki kuwa na Float kubwa kunafanya akaunti ya benki husika ilioko BoT kuwa na hela nyingi. Akaunti ya Benki ikiwa haina hela huko BoT basi hukopa hela kutoka benki nyengine ili kulipia Cheki za inward kwa niaba ya wateja wao.
Sababu nyengine inawezakuwa kupunguza float na ukiritimba wa mabenki chelewesha kuwalipa watu cheki zao. Float ni Cheki ambazo hazija mature, sasa benki yengine huongeza muda wa cheki ku-mature ili mteja asiweze kuchukua hela kwa haraka alafu Benki ipate muda mrefu wakuzitumia Hela hizo. Yani Benki ikiwa na float nyingi inakuwa vizuri kwao, wanaweza kuzitumia hizo hela kulipia cheki za inward (Cheki ambazo wateja wabenki hiyo walizolipa watu). Benki kuwa na Float kubwa kunafanya akaunti ya benki husika ilioko BoT kuwa na hela nyingi. Akaunti ya Benki ikiwa haina hela huko BoT basi hukopa hela kutoka benki nyengine ili kulipia Cheki za inward kwa niaba ya wateja wao.
Mafisadi ndo kama hivyo wanapelekwa jela, nadhani hiyo ndio njia yakudhibiti.
Post a Comment