Profesa Wamba Dia Wamba ambaye ni Kiongozi wa Pan Afrika Movement akiongea na wandishi wa habari hapa nchini Tanzania juzi, kuhusiana na maswala ya migogoro inayoendelea nchini Congo.
Soko la kifahari la Kariakoo chali kwa mapato sasa hivi limekuwa kama genge, kwani wafanyabiashara wengi hivi sasa wanashusha mizigo yao, katika soko la Kilwa lililopo Ilala. wafanyabiashara wa hapo waneiomba Serikali kuachia ngazi na kukabidhi mamlaka ya soko hilo kwa Manispaa ya ilala, kwani serikali imeshindwa kuendesha soko hilo na kusababisha hata wafanyakazi wanaofagia kushindwa kulipwa mishara yao.
Maafande hawa wa kike wakitafuta mitumba katika soko la Tandika kama wanavyooneka pichani.
Haya ndiyo maisha bora kwa kila Mtanzania , kijana huyo ambaye ni kuli katika soko la Temeke stereo akiwa amezidiwa na usingiuzi ulioambatana na ukosefu wa kazi akiwa amelala katika tenga la wafanya biashara ya Nazi, pole sana kaka yetu ndoo ukubwa huo.
Ngedere (tumbili) huyu anamwingizia mmiliki wake shilingi 60000, kila anapofanya onyesho katika mahoteli makubwa kama vile Jangwani Sea Breeze na Hoteli ya Giraff Hoteli zote za maeneo ya Mbezi Beach. Ngedele huyu ana uwezo wakunywa soda na anapewa amri kama binadamu. Kila wikiende ngedele huyu hufanya maonyesho katika hoteli hizo masaa mawili.
No comments:
Post a Comment