Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

December 6, 2008

Pichani ni OJ Simpson akiwa na nguo za kiraia.


Mchezaji mpira wa Marekani wa zamani bwana OJ Simpson amefungwa miaka kumi na tano (15) kwa makosa ya wizi wa kutumia nguvu (robbery), kupanga na kujaribu kuteka nyara (kidnap) na matumizi ya silaha kali(possession of deadly weapons). Mwenzake bwana Clearance Stewart pia amehukumiwa miaka kumi na tano (15). Wawili hao wanashutumia kuingia kwa nguvu kwakutumia silaha kali na kujaribu kuchukuwa baadhi ya picha, mipira na vifaa vyengine vya mpira kutoka kwa memorabilia dealers. Simpson alitaka kuchukua vifaa hivyo akisema ni mali yake.

Ikumbukwe kwa miaka ya tisini (90) Simpson alishinda kesi ya mauaji ambapo alishutumiwa kuwaua mkewe Nicole Brown Simpson pamoja na mpenzi wake Ronald Goldman (wote wakiwa wazungu). Kesi hii ilileta hisia kali kwa jamii ya watu weusi kule Marekani ambapo wengi waliona Simpson alikuwa anaonewa. Simpson aliposhinda kesi ilionekana kama ushindi kwa jamii ya watu weusi, huku jamii ya wazungu wakilaani maamuzi hayo.

Ni wazi kuwa sasa Simpson katika kesi hii yuko pekeyake hakuna mweusi anayetaka kumtetea. Wengi wanaona kifungo hichi ni stahili yake.

No comments: