HEEEEEEEEEE, msione watu wanatanua mitaani okaogopa sana picha hizi tatu zinawaonesha wazee hawa wa heshimi ambao wanafamilia zao zinazo waheshimu kabisa, je,hivi huwa wanaaga familia zao kuwa wanakwenda kazini? loo leo ndo usemi usemwao siku za mwizi ni AROBAINI umetimia.
Majambazi haya balaa, yakiwa katika picha tofauti kama zinvyo onyesha, walikamatwa katika hoteli ya Mtanzania iliyopo Tandale jijini, wakiwa na funguo bandia zijulikanazo kama Master key, baada ya kuingia hotelini hapo kama wateja kumbe walikuwa na mitego yao, walijua katika hoteli hiyo alikuwepo mtu mmoja mwenye vijisenti vyake, walimvizia akiwa amekwenda bafuni wakafungua mlango kwa funguo zao za bandia na kuchukua begi liliokua na hela.
Wahudumu wa hapo waliposhtuka, jamaa hao wakaanza kupata kipigo cha mbwa mwitu na baadaye polisi walikuja wakawapeleka kituo cha polisi Magomeni.
1 comment:
Aibu, jaamani, we need to protect our kids
Post a Comment