Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

December 3, 2008

ARRIVAL OF JOE THOMAS IN DAR

Hee kumbe Bongo iko hivi aka kama siamini , Joe Thomas akiwa amejishika kiunoni akishanga mambo ya bongo kulia ni Meneje wake.



Mabaunsa ambao ndio wenye Dhamana ya kumlinda Joe Thomas katikati wakisukuma masanduku ya msanii huyo.

Hata hili lipo hapa kwenu! hili ni gari lililo mbeba kutoka uwanja wa ndege hadi hoteli ya Kempinski Kilimanjaro.

Mwanamuziki wa miondoko ya R &B, kutoka nchini Marekani, Joe Thomas na wanamuziki wakongwe katika miondoko hiyo, Boyz 2 Men, wamewasili leo katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere wakitua na ndege ya Shirika la Ndege la Uganda majira ya saa kumi na moja na nusu jioni .

Msanii huyo ambaye amewasili jijini Dar, leo ilikuwa ni tofauti na mawazo na mitazamo ya mashabiki kiduchu waliojitokeza kwenye uwanja huo, wakitegemea kupata ushirikiano kutoka kwa mwanamuziki huyo kama inavyokuwa kwa wanamuziki mbalimbali waliowahi kufika nchini kwa ajili ya maonyesho kadhaa, jinsi wanavyokuwa charming. Lakini Joe Thomas alikuwa baridi sana, hata alishindwa kuwapungia mkono mashabiki hao kiduchu.

Uwanjani hapo walisikika mashabiki hao wakisema kuwa waliamua kufika uwanjani hapo ili angalau kumuona kwa sura kabla ya onyesho lake ambalo litafanyika viwanja vya Leaders Club, huku kiingilio cha onyesho hilo kikiwa ni kisichokidhi hali ya walalahoi.

"Angalau tumuone hapahapa kabla hajaingia leaders, kwani kiingilio chenyewe laki moja niitoe wapi, si bora nisake biashara ya kuifanyia kama ninayo laki yenyewe" alisikika mwanadada mmoja akisema hayo huku akitoa macho kuchungulia kwenye vioo vya milango ili kumuona wakati akiendelea na utaratibu wa kukaguliwa ndani.

Baada ya kuwasili aliingia moja kwa moja ndani ya gari aliloandaliwa na kuanza safari ya kuelekea hotelini na kuwaacha watu na waandishi waliofika uwanjani hapo kwa ajili ya mahojiano wakibaki wameduwaa na kuulizana kuwa kuwekwa kote na masaa yote haya uwanjania hapa mambo yenyewe ndo haya? hata ushirikiano hakuna? baada ya hapo kila mmoja alichukua ustaarabu wake na kutokomea kila mmoja njia yake.

3 comments:

Anonymous said...

jamaa kumbe ana maringo.

Anonymous said...

hawezi kuchekea kila mtu kwani amekuwa zezeta wabongo bwana. jua kwamba jamaa amechoka na safari ndefu kisha nchi yenyewe joto na airport ni local. mpeni muda atato burudani.

Anonymous said...

wabongo tumo na sisi,mzuka wa holliday umeshaanza kama huna kilo shauri lako.