Hapa samaki wako tayari kwa mkarangizo, huyu samaki mkubwa anaitwa Changu hapa Bongo wakati Msa anaitwa Kolekole . Hawa samaki wadogo wanaitwa Tasi hapa Bongo wakati Msa wanaitwa Tafi.
Yani hapa Ferry kuna huduma kama hii hapa, vijana wanakungenezea samaki yani kupaa samaki (Mombasa wanaita kupara samaki) kwa bei nzuri ya maelewano. Kuna vijana wasiopungua hamsini kwa shughuli hii.
Ukienda kununua samaki usiende kichwa kichwa utaumia, hapa mbele ni sehemu ya mnada samaki ni bei che na hata hawa wauza samaki hapa sokoni hununua hapo. Lakini kuwa makini kuna minada feki hubuniwa pale pale, na bei huwa zakuchanganya wateja mfano (sabini na tano, sasa huwezi kujua kama ni 75,000 au 7,500) kisha wanaende fasta fasta basi huwa ni balaa. Just be carefull.
November 3, 2008
Mambo ya kushangaa Ferry (Soko la samaki), Dar es salaa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment