Pages

January 27, 2010

Offside Trick Watamba Sana Katika Anga Za Mduara (Chakacha)

Kundi la mduara la Offside Trick hivi karibuni limekuwa maarufu sana katika siku za karibuni na hii ni baada ya kutoa nyimbo zao mbili mpya zenye ujumbe tata ziitwazo; Samaki na Al bata. Kundi hili kutoka Zenji limekuwa likishirikisha wanamuziki maarufu kutoka huko kisiwani kama vile Mzee Yusuph na wengine.

Ndani ya video ya Al bata Mzee Yusuph anaonekana akiimba ilhali anaangilia bata huku mate yanamdondoka. Kama hauoni bata kwenye hiyo picha basi? "Kwaheri".

Moja ya ujumbe kwenye nyimbo hiyo ya Al bata unasema; "Nyama ya mbele ni kavu ya nyuma ina mafuta". Sasa sijui wanamaanisha nini ila sidhani kama ni mambo ya stori ya "Uncle Jambazi"

Pwani bila jahazi au kidau si pwani.

Mzee Yusuph Mwenywe.

6 comments:

  1. Anonymous9:02 AM

    Uncle jambazi ndio nani tena huyo.

    ReplyDelete
  2. Mbongo3:57 PM

    vijana hawa wanatupa burudani ya mwaka, mimi binafsi wanaukonga moyo wangu shwadakta kabisa.

    ReplyDelete
  3. Anonymous6:52 PM

    Stori ya ankal jambazi ni kali sana.

    ReplyDelete
  4. Anonymous9:45 AM

    Nyimbo nzuri, sauti nzuri, maneno === matusi ===

    siwezi kutizama video hiyo pamoja na dada , binti , baba yangu
    maneno kama yule hanisi anasema "" nataka kutiwa ? "" au nyama ya ya nyuma ina mafuta ??? AIBU
    NYIMBO HIZI NI VIGUMU KUSIKILIZWA NA HADHARA YA WATU WANAOJIHESHIMIWA

    ReplyDelete
  5. Anonymous11:40 AM

    Jamani hii nyimbo ni aibu tupu...mdundo mzuri,sauti ya mwimbaji nzuri...LAKINI.....maneno ya nyimbo ni matusi matupu..khasara kubwa hii

    ReplyDelete
  6. Anonymous11:40 AM

    Jamani hii nyimbo ni aibu tupu...mdundo mzuri,sauti ya mwimbaji nzuri...LAKINI.....maneno ya nyimbo ni matusi matupu..khasara kubwa hii

    ReplyDelete