Pages

September 29, 2009

Miss Vodacom Tanzania 2009 Kufanyika Ijamaa Hii.

Warembo ishirini na tisa wanaowania taji la Vodacom miss Tanzania mwaka huu 2009 litakalofanyika Ijumaa ya tarehe 2 oktoba katika ukumbi wa Mlimani City wakiwa katika picha ya pamoja katika Hotel ya Girrafe wakati wa sherehe ya siku ya wandishi wa habari walipotembelea kambini kwao.

Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania wakiwa wamemzunguka mwandishi wa habari wa Gazeti la Dimba linalomilikiwa na New Habari akiwapa maelezo kuhusiana na wandishi wa habari wakati wa siku ya Media day.

Mzee wa Mjengoni mzee wa kuchana Jimmy akiwa katika pozi la hatari na mrembo anayewania nafasi ya Vodacom Miss Tanzania Sylvia Shally ambaye ndiye marikia wa urembo wa Ilala mwaka huu.

Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi akifanya mahojiano na Baadhi ya warembo wanaoshindania taji la Vodacom Miss Tanzania 2009.

Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania George Rwejuna akimkabidhi zawadi ya ushindi wa kuvua samaki kwa upande wa wanawake Linda Wiechers( kulia ) ambaye ni mama wa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Dietrlof More hayupo pichani, katikati ni kiongozi wa Yacht Club Spiros Manoloudi Conmodore. Mashindano hayo ya maboti yalifanyika katika kisiwa cha Sinda yakiwa yamezishirikisha nchi Nne ,Tanzania, Kenya, South Africa na Zimbabwe.

1 comment:

  1. Anonymous1:17 PM

    Nakubali safari hii mambo yameiva.

    ReplyDelete