Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

July 20, 2009

Pearson Longman yaendesha mafunzo kwa waalimu 600

Kampuni inayojihusisha na uchapishaji wa vitabu ya Pearson Longman, wiki iliyopita iemeanza kuendesha mafunzo ya masomo ya Hisabati na Lugha kwa walimu wa shule za msingi za wilaya za Kinondoni na Ilala. Meneja Kuu Kampuni hiyo, Anitha Rwehumbiza alisema jana Jijini kwamba lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha waalimu kupata uelewa mkubwa wa masomo hayo. Alisema mafunzo hayo yanayoendeshwa kwa pamoja na Taasisi ya Pearson Longman yenye Makao Makuu yake nchini Uingereza yanatarajiwa kudumu kwa mwezi mmoja. Anitha alifafanua kwamba mbali na Wilaya hizo kupata elimu hiyo, tayari waalimu katika Wilaya ya Temeke wameshafaidika na mafunzo hayo. Alisema waalimu 640 wa shule mbalimbali za Wilaya hiyo wanatarajiwa kupata mafunzo hayo ambayo yatawajengea uwezo mkubwa wa uelewa wa masomo hayo.

Naye Afisa Taaluma wa Wilaya ya Ilala (Shule za Msingi) Joyce Senkoro, aliipongeza kampuni hiyo kwa kuendesha mpango huo ambao alisema una manufaa makubwa sana kwa taifa hili. “Mpango huu una manufaa sana na nimewaomba waalimu watambue kwamba mafunzo haya si kwa ajili yao bali ni kwa shule wanazotoka, hivyo wahakikishe kwamba ujuzi wanaoupata” Alisema kwamba serikali inafarijika sana inapoona sekta binafsi inashiriki katika masula ya kukuza elimu hapa nchini. Alisema serikali kwa upande wake itaendelea kuwaunga makono watu wenye moyo wa kukuza elimu hapa nchini na kwamba elimu ni muhimu kwa maendeleo ya taifa letu.

No comments: