Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

April 8, 2009

HALI KATIKA SOKO LA MBAGALA

Wafanyabiashara katika Soko la nafaka la Mbagala Rangi Tatu,wapo katika hali mbaya baada ya Manispaa ya Temeke kushindwa kuweka miundo mbinu katika soko hilo. Soko hilo lenye mita za mraba 100x100 linajumla ya wafanyabiashara zaidi ya 1000, soko lina wafanyakazi wawili ambao hawakidhi kutunza mazingira ya soko hilo.




Akiongea na mwandishi wa habari hizi Katibu Mkuu wa soko hilo Frenk Mapolu alisema kuwa soko hilo limekuwa na uchafu kutokana na Manispaa kushidwa kuwajibika ipasavyo kwani viongozi wa soko wamekuwa wakijitahidi kadiri ya uwezo wao. Manispaa wamekuwa wakikusanya Mapato ya shilingi 50,000. kwa mwezi lakini wameshindwa kabisa kutoa huduma ya kiafya. Alifafanua ukifika katika mabanda ya kuchinjia kuku utkakuta mashimo yanatoa maji machafu kutokana na kukosa sehemu ya kwenda pia Dampo limejaa maji lakini hawataki kuja kuyanyonya pomoja na kuwa dampo hilo limechimbwa kwa nguvu za wanasoko wenyewe kwa kiasi cha shilingi 1,500,000.

Pia wafanyabiashara hao kupitia viongozi wa soko hilo walipeleka pendekezo la mabaoresho ya soko kwa kujengwa soko la kisasa ikiwa ni pamoja na kuiomba manispaa kutoa mapendekezo ya mchoro wa soko la kisasa lakini hadi hivi sasa hakuna kitu kama hicho. Uboreshani wa soko hilo unategemea kugharimu kisai cha shilingi milioni 250,000,000 ambazo tayari manispaa wameshapelekewa mapendekezo hayao.


Jinsi samaki wanavyo pikwa sokoni hapo.

No comments: